loading . . . DRC: Mapigano yanaendelea Kivu Kusini kabla ya mkutano kati ya Marais wa Kongo na Rwanda Mapigano yameendelea leo Jumatano asubuhi, Desemba 3, katika mkoa wa Kivu Kusini. Hali bado ni tete katika maeneo kadhaa huko Uvira, Walungu, na Kabare. Mapigano hayo yanahusisha AFC/M23, jeshi la Kongo, makundi ya Wazalendo, na, kulingana na muktadha wa eneo hilo, vikosi vya Burundi. Kuibuka tena kwa vurugu kunakuja huku Félix Tshisekedi na Paul Kagame wakitarajiwa kusaini makubaliano ya amani huko Washington siku ya Alhamisi, mbele ya Donald Trump. https://rfi.my/CEjc.bs